“Watapaa juu kwa mbawa kama tai...” — Isaya 40:31
Tai ni ndege mwenye nguvu, maono makali, na ujasiri wa kipekee. Anapokutana na dhoruba, haikimbii - hutumia upepo mkali wa dhoruba hiyo kupaa juu zaidi.
Hii ni picha ya mtu anayemtegemea Mungu: badala ya kukata tamaa, huinuliwa zaidi katikati ya changamoto.
Unaweza kuwa kwenye hali ngumu sasa, lakini kwa imani, unaweza kuinuliwa juu zaidi ya hofu, huzuni na mashaka.
Usiogope dhoruba - inaweza kuwa daraja lako la kuinuliwa.